Dhambi ni uasi, 1Yoh 3:4; Isa 1:2; Zab 51:4; Kum 9:18.
Dhambi
inaweza kutokea kwa namna mbalimbali kuanzia kwa matendo maovu, kwa
makusudi mpaka kwa bahati mbaya, kwa sababu ya udhaifu, uvivu au
kutokujua, Kut 32:30; Mt 5:22,28; Mit 28:13; Rum 1:29-32, 3:23; Yak
4:17.
ASILI YA DHAMBI
Kutokana na shughuli za shetani katika
bustani ya Edeni inaonekana wazi kuwa dhambi ilikuwapo ulimwenguni kabla
ya Adamu na Hawa hawajatenda dhambi, lakini Biblia haielezi jinsi
dhambi ilivyoanza kwa asili yake bali inaeleza tu jinsi ilivyoingia kwa
mwanadamu. Mwanadamu alivuka mpaka ambao Mungu alimwekea, hivyo
alianguka katika dhambi. Kiburi kilikuwa kiini cha dhambi ya mwanadamu,
1Yoh 2:16; Rum 1:21-23.
Dhambi ilingia kwa sababu mwanadamu alianza
kumtilia mashaka Mungu, Yak 1:14. Dhambi ilianzia moyoni mwake na tendo
la kutokuamini lilikuwa matokeo yake ya lazima, Yer 17:9; Mwa 6:5.
MATOKEO YA DHAMBI
Mwanadamu alianguka chini ya hukumu ya Mungu na kuingia hali ya uadui dhidi ya:-
1. Ulimwengu wa viumbe, Mwa 3:17-19.
2. Wanadamu wenzake, Mwa 3:12,13; 1Yoh 3:12.
3. Nafsi yake mwenyewe, Mwa 3:7, 11-13; Rum 7:15,19.
4. Mungu, Mwa 3:8-10, 22-24; Rum 3:10-18.
Adhabu
kuu ya dhambi ni mauti, Mwa 2:17; 3:19,24; Rum 6:23. Mauti haikuwa ya
kimwili tu bali pia ya kiroho, ambayo ni kutengwa na Mungu ambaye ni
asili ya chemchemi ya uzima wa kiroho, Rum 6:16,17, 5:13; 1Kor 15:56.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni