1. Upendo ni zile hisia unazozipata wakati unapokutana na mtu unayeshabihiana naye.
2. Upendo ni kitendo cha msamaha usio na kikomo na kujali ambako huwa tabia.
3. Upendo ni mshikamano ambao hutokana na imani iliyojengeka ndani ya mtu juu ya mazuri ya mtu fulani.
AINA ZA UPENDO
Kuna aina nne za upendo; ambazo ni:
1. Eros
2. Philia
3. Storge
4. Agape
UPENDO WA EROS
Huu ni upendo wa tamaa kati ya mke na mume, Wim 3:1,4.
UPENDO WA PHILIA
Huu
ni upendo wa kirafiki. Katika lugha ya kyunani, uupendo huu umejikita
sana katika '' NIPE NIKUPE'' ambapo watu wawili wananufaishana, 1Sam
18:1-3; Yn 11:11.
UPENDO WA STORGE
Huu ni upendo wa kifamilia au ndugu kati ya baba, mama, kaka na dada, Yn 11:3, 21.
UPENDO WA AGAPE
Huu
ni upendo wa ngazi ya juu, wa Kimungu usio na ubinafsi, wenye kujitoa,
usio na kikomo, usio na masharti, hauhitaji kupata chochote toka kwa
yule umpendaye. Ni upendo ambao Mungu anatutarajia kuuonesha katika
ulimwengu huu. Yn 3:16.
TABIA ZA UPENDO
1. Haupungui neno lolote, unaenda popote ambako wengine hawathubutu kuenda, hutoa uhai wake, 1Kor 13:8.
2. Huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote, 1Kor 13:7.
3. Haufurahii udhalimu, hufurahi pamoja na kweli, 1Kor 13:6.
4. Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya, 1Kor 13:5.
5. Hufadhili, hauhusudu, hautakabari, haujivuni, 1Kor 13:4.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni