Jumamosi, 3 Mei 2014

KUTEMBEA KATIKA ROHO




Gal 5:25
i.        Kutembea katika Roho ni kutekeleza maamuzi ya Roho na kuishi ndani ya mwongozo wake na si kuenenda au kuingiza au kujaribu kurekebisha au kubadilisha mwongozo.
ii.      Kutembea katika Roho ni kufanya mambo yale ambayo torati na mwili vimeshindwa kuyafanya.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUTEMBEA KATIKA ROHO
1.    UJUE UDHAIFU WAKO, Yak 3:2
Jambo hili ni la muhimu sana na kamwe halipaswi kupuuzwa. Unatakiwa kuubaini udhaifu wako kwa sababu kweli iliyomo ndani yako ni adui na inaujua udhaifu wako kuliko wewe. Lielewe eneo hili kwa makini na umkabidhi Roho Mtakatifu ambaye ni rafiki mwema na mnasihi wa milele naye atakutia nguvu na kukusaidia kuutambua na kuzuia majaribu na vishawishi.
2.    YAFISHE MATENDO YA MWILI KWA ROHO, Rum 8:3
Mtu ambaye amefanywa upya na Roho hawezi kunaswa katika dhambi. Kwa Roho, tamaa za mwili zinashindwa. Kuyafisha matendo ya mwili ni adhimu ni sawa na kusema “dhambi hapana” lakini ni tofauti na kampeni ya kupambana na madawa ya kulevya miongoni mwa vijana miaka mingi iliyopita. Kusema “dhambi hapana” pekee haitafanikiwa, kusema “dhambi hapana kamwe huwezi ukashinda dhambi. Je nini unatakiwa ufanye? Sema “hapana Kwa Roho.
3.    UONGOZWE NA ROHO, Rum 8:14; Efe 5:15
Roho mtakatifu hutuongoza wakati wote. Hutuongoza kupitia neno lake lililofunuliwa kwa manabii, 2Pet 1:20, 21. Tunapaswa kuwa waangalifu, waombaji na wanyenyekevu katika kutumia hekima pana ya Biblia katika hali tunazokutana nazo. Wakati mwingine Roho Mtakatifu hutuongoza moja kwa moja. Roho Mtakatifu anaweza kutenda kwa njia yoyote, kulingana ratiba yoyote kama apendavyo. Hatumwongozi namna au wakati gani atembee. Biblia imebainisha mifano mingi ya jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kutenda, tunapaswa kukubali kuwa wakati mwingine aweza kuchagua kutuongoza moja kwa moja kama tutakuwa huru na tu katika mwongozo wake.
4.    UJUE U BABA WA MUNGU  KWA ROHO Rum 8:15-17
Pasipo Roho Mtakatifu tusingeujua utambulisho wetu kuwa tu wana wa Mungu. Ashukuriwe Mungu aliyetupatia Roho Mtakatifu bure, na mistari hii kutoka Rum 8 inaonesha mambo matatu ya ajabu ambayo Roho Mtakatifu ameyafanya:
a.    Anatenda kama kiunganishi ambaye ametutoa mahali pa utumwa na hofu na kutuleta mahali pa kupitishwa na kukubaliwa.
b.    Anatusaidia kulia “ABBA” yaani baba.
c.    Anashuhudia na roho zetu kuwa tu wana wa Mungu.
5.    OMBA KATIKA ROHO, Rum 8:26-28
Mistari hii miwili (Rum 8:26,27)  ina utajiri mwingi na inatusaidia katika kuishi kwetu katika Roho.
a.    Tunajifunza kuwa tu dhaifu tunapokuwa katika kuomba. Hatujui kuomba katika hali yoyote.
b.    Tunajifunza kuwa Roho huungana kutusaidia tunapotaka kujua jinsi ya kuomba kwa ktuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
c.    Roho huchunguza mioyo yetu na kujua akili zetu kwamba zimeelekezwa kwake hata kama hatujui namna ya kuomba.
d.    Matokeo ni kwamba maombi yetu yanaomba “kulingana na mapenzi na Mungu”  kwa sababu Roho Mtakatifu (anatembea katikati yetu) anatuongoza kuomba na kuyawasilisha maombi yetu kwa baba.
FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA ROHO
1.    Kuwekwa huru mbali na sheria ya dhambi na mauti, Rum 8:2-4.
2.    Kuwa hekalu la Roho Mtakatifu, 1Kor 6:19.
3.    Kuyajua mafumbo ya Mungu, 1Kor 2:10-15.
4.    Kushirikishwa uzima wa milele, Yn 3:5; Efe 2:5.
5.    Kuongozwa na roho, Lk 2:25, 26; Mdo 13:4, 16:6-10.
6.    Kuthibitishwa kuwa wana wa Mungu, Rum 8:16.
7.    Roho Mtakatifu kusema nasi, Mdo 10:19.
8.    Kuwa mashahidi, Mdo 5:32; Yn: 16, 17.