Roho mtakatifu ni nafsi ya tatu katika uungu.
A: JINSI
TUHAKIKISHAVYO KUWA ROHO MTAKATIFU NI NAFSI MOJA
1. Roho Mtakatifu
anadhihirishwa kuwa na akili na hekima
- Anaelimisha watu wa
Mungu, Neh 9:20.
- Anafundisha
wakristo, Lk 12:11, 12.
- Anakumbusha yote, Yn
14:26.
- Anatoa karama za
hekima na maarifa, 1Kor 12:8.
2. Roho Mtakatifu
anajionea mambo mbalimbali peke yake
- Nia yake haipatani
na nia ya mwili, Rum 8:6.
- Anaweza kuhuzunika
na kuhuzunishwa, Isa 63:10.
- Anatutamani kwa
utakatifu kiasi cha kuona wivu, Yak 4:5, 6.
- Akikufuriwa hakuna
msamaha, Mt 12:30, 31.
3. Roho Mtakatifu
anakuwa na mapenzi na kusudi lake
- Akigawa karama zake
, anatenda kama apendavyo, 1Kor 12:11.
4. Roho Mtakatifu
anasema na watu
- Alimwambia Filipo
kusogea karibu na gari la Mkushi, Mdo 8:29.
- Alimwambia mtume
Petro kuondoka, Mdo 10:19, 20.
- Alitabiri kwa midomo
ya Agabo, Mdo 21:10, 11.
- Anasema na
watakatifu wenye masikio, Ufu 2:7.
5. Roho Mtakatifu
anaomba
- Mwenyewe ni Roho wa
neema na kuomba, Zek 12:10.
- Anawaombea
watakatifu kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, Rum 8:26.
- Ametumwa kulia
“ABBA” ndani ya wana wa Mungu, Gal 4:6.
6. Roho Mtakatifu
anaongoza
- Alimwonya na
kumwongoza Simeoni, Lk 2:25, 26.
- Aliwaongoza
watumishi wa Mungu, Mdo 13:4.
- Aliwakataza na
kuwapa maono akina Paulo na Timotheo, Mdo 16:6-10.
7. Roho Mtakatifu
anachunguza na kushuhudia
- Anachunguza mafumbo
ya Mungu, 1Kor 2:10-13.
- Mwanadamu hawezi
kujiepusha naye, Zab 139:7.
- Atushuhudia wokovu.
B: TABIA YAKE ROHO MTAKATIFU
Roho Mtakatifu anatajwa kwa majina
mbalilmbali katika Biblia ambayo maana yao yanafunua tabia yake wazi.
1. Ndiye Roho wa Mungu
- Alikuwapo wakati
dunia inaumbwa, Mwa 1:2.
- Alikuwapo wakati wa
kutolewa maandiko, 2 Pet 1:20, 21.
- Alikuwapo wakati wa
kutungwa mimba kwa Mariamu, Mt 1:18.
2. Ndiye Roho wa kweli
- Anasimama kwenye
kweli yote, Yn 14:17.
- Anapinga na
kudhihirisha uongo wote, Mdo 5:1-3.
- Watakatifu
wanamtambua na kujazwa tabia naye, Yn 14:17.
3. Ndiye Roho Mtakatifu
- Mwenyewe ni
mtakatifu na anawatakasa wale ambao wanamtii Mungu, 1Thes 4:7, 8; 1 Pet 1:2.
4. Ndiye Roho ufunuo
- Anajua yote kabisa,
mtu hawezi kujiepusha naye, Zab 139:7.
- Anachunguza yote,
hata mafumbo ya Mungu, 1 Kor 2:10.
- Anataka kuwapa
watakatifu hekima ya ufunuo katika kumjua pamoja na yote waliyopewa ndani ya
Kristo, Efe 1:17, 18.
- Anafunua
yatakayotokea mbeleni, Ufu 1:9-11; Yoe 2:28.
5. Ndiye Roho wa upendo
- Tabia yake ni
upendo, na anataka kuwajaza wakristo upendo wake, 2 Tim 1:7.
6. Ndiye Roho wa
hekima, shauri, uweza, maarifa na kumcha Bwana
- Roho huyo alikaa juu
yake Yesu, Isa 11:1-2.
7. Ndiye Roho wa
utukufu
- Anawakalia wale wanaolaumiwa
kwa ajili ya jina lake Yesu, 1 Pet 4:14; Mdo 6:10, 15.
- Akipata kutawala
katika maisha ya mkristo, inatokea kuwa mkristo huyo anabadilishwa na kufanana
na Bwana toka utukufu hata utukufu, 2 Kor 3:18.
C: ROHO MTAKATIFU KWA
MIFANO YAKE
Mifano inatumiwa ili kusaidia kuelewa mambo
zaidi. Kwa kuwa Roho Mtakatifu hana umbo
la binadamu, anaoneshwa katika Biblia kwa mifano mbalimbali kusudi tumwelewe
jinsi alivyo.
1. Roho Mtakatifu
alijifunua akishuka kama HUA
- HUA ni ndege mzuri ,
anapendeza na ni mpole, Mt 3:16.
- Roho Mtakatifu
aliposhuka kama HUA anaonesha uzuri, mapenzi, wema na usafi, Zab 143:10.
2. Roho Mtakatifu
alitokea kama MOTO
- Moto huangaza na
kufunua, hupima na kuyeyusha, hubagua na kupambanua, husafisha, kubadilisha na
huunganisha, ndivyo alivyo Roho Mtakatifu katika uweza wake, Mdo 2:3, 4.
3. Roho Mtakatifu anafanana na UPEPO
- Upepo huvuma
upendako bila kuonekana wala kuzuiwa na mtu, sawasawa na Roho Mtakatifu katika
kazi zake. Haongozwi na mtu kwa sheria yake, anatenda mwenyewe kama apendavyo,
Mdo 2: 2-4; Yn 3:8, 9.
4. Roho Mtakatifu
anatokea kama CHEMCHEMI ya maji
- Maji yana nguvu ya
kuondoa kiu kwa mtu, kadhalika Roho Mtakatifu ana uwezo wa kuondoa kiu ya
kufanya maovu kwa mtu, Yn 7:37-39.
5. Roho Mtakatifu ni
kama MAFUTA
- Mafuta hurainisha,
hurahisisha, hudumisha, huponyesha na huwezesha, Mdo 10:38.
- Mafuta ni mfano wa
uzima wa milele katika Roho wa Mungu, Mt 25:3-8.
- Mafuta ni mfano wa
shangwe katika haki, Ebr 1:9,1 0.
- Mafuta ni mfano wa
umoja na upendo ambao unaonekana kati yao waongozwao na Roho Mtakatifu, Zab
133: 1, 2.
6. Roho Mtakatifu
ameitwa MUHURI
- Muhuri huthibitisha
na hudhihirisha haki au uhalali wa kitu au mtu, 2 Tim 2:19.
7. Roho Mtakatifu
anapokewa kama ARABUNI
- Watakatifu wamepewa
kama arabuni mioyoni mwao, wana hakika juu ya urithi wao, 2Kor 1:21, 22; Efe
1:14, 15.
D: HABARI ZAIDI JUU YA KAZI ZAKE ROHO
MTAKATIFU
Roho Mtakatifu anafanya kazi muhimu sana
katika ulimwengu, katika maisha ya mkristo na katika kanisa kwa ujumla.
1. Roho Mtakatifu
anauhakikishia ulimwengu
- Kwa habari ya dhambi,
Yn 16: 9.
- Kwa habari ya haki,
Yn 16:10.
- Kwa habari ya
hukumu, Yn 16:11.
2. Roho Mtakatifu
anamshirikisha mtu uzima wa milele
- Roho Mtakatifu
anaumba uzima wa milele ndani ya roho ya mtu aliyezaliwa mara ya pili, Yn 3:5;
Efe 2:5.
- Wanaomwani Yesu wanaishi na kuenenda kwa Roho wa Mungu, Gal 5:25.
3. Roho Mtakatifu
anamwacha mwanadamu huru na sheria ya dhambi na mauti
- Kwa maana sheria ya
Roho wa uzima inamwacha huru mbali na sheria ya dhambi, Rum 8:2-4.
- Tena hakuna hukumu
ya adhabu juu yao walio katika Kristo, wamekwisha kuhuishwa rohoni, tena
watahuishwa kwa mwili pia watakapofufuka kwa nguvu ya Roho, Rum 8:1, 8-11.
4. Roho Mtakatifu
anamshuhudia anayemwamini Yesu kuwa ni mtoto wa Mungu
- Roho Mtakatifu
hushuhudia na roho zetu kuwa tu wana wa Mungu, Rum 8:16.
- Roho Mtakatifu anamshuhudia
mkristo udugu naye Kristo mwana wa
Mungu, Gal 4:6.
5. Roho Mtakatifu
anawapa wakristo nguvu
- Anawapa watu wa
Mungu nguvu kwa utu wa ndani, Efe 3:16, 17.
- Anawapa nguvu ya
kuwa mashahidi wake Kristo, Mdo 1:8, 9.
- Anawapa nguvu ya
kuwa waaminifu hata kufa, Mdo 7: 54-58.
6. Roho Mtakatifu
anawakumbusha walioamini yote aliyosema Yesu
- Atawakumbusha yote,
Yn 16:13-15.
7. Roho Mtakatifu
anawajaza walioamini shukrani na shangwe
- Roho Mtakatifu
anawapa wakristo nyimbo na tenzi nzuri, Efe 5:18-20.
- Anawawezesha kuimba
na kusema kwa moyo wote, Zab 86:12, 13.
- Anawajaza furaha
hata wakifungwa na kuteswa, Mdo 16:25-33.
8. Roho Mtakatifu ni
msaidizi wa walioamini
- Anawasaidia kuyajua
waliyokirimiwa na Mungu katika Kristo, 1Kor 2:12.
- Anawasaidia katika
mambo ya kiroho, 1Kor 2:13
- Anawasaidia katika
udhaifu, Rum 8:26.
- Anawakumbusha yote
aliyosema Yesu, Yn 14:26.
9. Roho Mtakatifu
anamtukuza Yesu mwana wa Mungu
- Anawaongoza katika
kweli yote na kumtukuza Yesu, Yn 16:13, 14.
E: UBATIZO KATIKA ROHO MTAKATIFU
1. Mungu ametoa ahadi
juu ya ubatizo katika Roho Mtakatifu
- Ahadi hii ilinenwa
zamani zile za nabii Yoel, Yoel 2:28-32.
- Yesu mwenyewe
aliwaahidi wanafunzi wake, Yn 16:7; Mdo 1:8.
2. Mambo yaliyokuwa ya
lazima kutimia kabla ya ubatizo katika Roho Mtakatifu kutokea ulimwenguni
- Ilimbidi Yesu Kristo
kuja ulimwenguni kwanza, Gal 4:4-6.
- Ilimbidi Yesu kufa
msalabani kusudi upatanisho kati ya wanadamu na Mungu upatikane, 1Tim 2:5, 6;
Ufu 5:9, 10.
- Ilimbidi Yesu
kufufuka na kuondoka duniani akapandishwa mbinguni, Mdo 2:32, 33; Yn 16:7.
3. Maana yake
“Kubatizwa katika Roho Mtakatifu”
Neno
hili ‘ubatizo’ linatoka katika lugha ya kiyunani yaani ‘BAPTISMA’ maana yake ni “kuzama
au kuzamisha”.
Kwa hiyo kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni harakati za utendaji kazi wa Roho
Mtakatifu juu na au ndani ya muumini ambapo anakuwa amejazwa uwezo na nguvu
maalumu.
- Kuna tofauti kati ya
kuzaliwa kwa Roho mara ya pili na kubatizwa katika Roho Yule mmoja.
Yaani ni hivi:
Katika
kuzaliwa kwa Roho mara ya pili ni kwamba mtu anaumbwa upya kwa
uzima wa milele,
Yn 3:5-8, ambapo kubatizwa katika Roho ni kujazwa uwezo na nguvu maalumu, Lk 3:16, 17.
Yn 3:5-8, ambapo kubatizwa katika Roho ni kujazwa uwezo na nguvu maalumu, Lk 3:16, 17.
- Kubatizwa katika
Roho Mtakatifu ni kupokea nguvu ya ajabu na kuwa mashahidi wa Yesu Kristo
duniani, Mdo 1:8.
- Kubatizwa katika
Roho Mtakatifu kunaleta ujasiri wa kumshuhudia Yesu kuwa Bwana na Mwokozi, Mdo
4:8
- Kubatizwa katika
Roho Mtakatifu kunaleta karama, 1Kor 12:4-12, Mdo 10:46.
- Mtu akijazwa Roho
Mtakatifu anajazwa an upendo wa Mungu, Rum 5:5, 6.
4. Habari ya kuupokea
ubatizo katika Roho Mtakatifu
- Waliozaliwa mara ya
pili, wenye moyo safi, wanaomtii Mungu ndio wanaweza kuupokea ubatizo katika
Roho Mtakatifu, Yn 14:17; Mdo 5:32; 8:18-21; 15:7-11.
- Ahadi hii ni kwa
ajili ya wakristo wote wa siku za mwisho, Mdo 2:39.
5. Kufanywa upya na
kuenenda katika Roho Mtakatifu na nguvu zake
- Ubatizo katika Roho
Mtakatifu unafungua mlango wa mkristo kujaa nguvu na uweza kila wakati akiishi
nuruni maishani mwake, Yn 7:38; Mdo 6:5.
- Kubatizwa katika
Roho Mtakatifu ni mwanzo wa kuenenda katika ushindi, 2Kor 4:16, 3:18.
- Kubatizwa katika
Roho Mtakatifu unapokewa mara moja tu katika maisha ya mtu, Zab 51:10-12; Rum
11:29.
F: KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Nyakati zilizopita Roho Mtakatifu
alijidhihirisha duniani kwa namna mbalimbali, lakini kwa wakati huu wa mwisho
anajidhihirisha hasa kwa karama zake katika kanisa. Matokeo haya yana maana
sana katika kazi ya kuieneza injili na kuyatimiza mapenzi ya Bwana.
1. Tupambanue KARAMA ZA
ROHO na karama zingine zitokazo kwa Mungu
- Wokovu na uzima wa
milele ni karama za Mungu walakini haina maana sawa na karama za Roho
Mtakatifu, Rum 6:23.
- Kula na kunywa ni
karama ya Mungu walakini maana yake si sawa na karama za Roho Mtakatifu, Mhu
3:13.
- Roho Mtakatifu
mwenyewe pamoja na matokeo yake yote yameitwa KIPAWA kwa jumla, walakini maneno
haya matatu KARAMA ZA ROHO yanahusu kitu cha pekee ndani yake, Mdo 2:38.
- KARAMA ZA ROHO ni
karama ambazo mkristo anapokea akiwa anabatizwa ubatizo wa Roho Mtakatifu tu.
Ni karama za uwezo wa pekee,tena haziwezi kuwepo kwa njia zingine, 1Kor 12:4.
- Mkristo anaweza
kutumika kweli katika karama hizo kwa njia ya ufunuo wa roho tu, 1Kor 12:7, 8.
2. Pana tofauti za
KARAMA ZA ROHO
- KARAMA ZA ROHO
zinahesabiwa na kutajwa kuwa ziko tisa (9) kwa idadi yake, 1Kor 12:4-9.
I.
Neno la hekima
II.
Neno la maarifa
III.
Imani
IV.
Karama za kuponya
V.
Matendo ya miujiza
VI.
Unabii
VII.
Kupambanua roho
VIII.
Aina za lugha
IX.
Tafsiri za lugha
I.
KARAMA YA NENO LA HEKIMA
- Ni elimu kutokana na
ufunuo wa roho, hutumiwa wakati wa mahitaji yake, Mdo 6:9, 10, 1Kor 2:6, 7.
- Karama hii
inawasaidia viongozi waliowekwa na Mungu kuliongoza kanisa lake, Mdo 6:2, 3.
- Kwa karama hii, Roho
alishirikiana na mitume katika kukata shauri, Mdo 15:28.
II.
KARAMA YA NENO LA
MAARIFA
- Karama hii
inawawezesha walioitwa na Mungu kufundisha neno lake, 2Tim 2:15.
- Inawawezesha kuelewa
uhusiano uliopo kati ya agano la kale na agano jipya, Mdo 2:15, 16.
III.
KARAMA YA IMANI
- Sivyo kuwa na imani
ya kuupokea wokovu bali hii ni imani maalum inayoletwa na Roho, kusudi jina la
Yesu litukuzwe kwa ishara zinazofuata tendo la imani hiyo. Matokeo yake
yanajenga kanisa katika kumtegemea Yesu zaidi, Mk 16:18; 1Kor 13:2.
IV.
KARAMA ZA KUPONYA
- Karama za kuponya
siyo elimu ya uganga kwa kusoma shuleni, bali ni matokeo na uwezo katika Roho
Mtakatifu, Mdo 3:4-9.
V.
KARAMA YA MATENDO YA MIUJIZA
- Kutoa pepo wachafu,
Mdo 8:6, 7.
- Wafu kufufuliwa, Mdo
9:40.
- Kulipiza kisasi, Mdo
13:9-11.
VI.
KARAMA YA UNABII
Neno hili
limetafsiriwa kuwa ni KUHUTUBU kwa Kiswahili, maana yake ni KUTABIRI
au KUSEMA
KWA UNABII, yaani si kuhutubu kwa njia ya kujitayarisha mwenyewe au
kwa kusudi
la mtu, bali ni kwa kujaliwa na Roho, 1Kor 14:1.
- Unabii wa karama za
roho unaweza kutokea:-
i.
kwa kufunua wazi mambo yaliyokwisha kufanyika katika siri,
Mdo 5:1-5.
ii.
tena kwa kuyafunua yatakayotukia mbeleni, Mdo 11:27, 28.
- Unabii wenyewe
unatolewa kwa njia mbili, yaani:-
i.
mara moja, neno kwa neno jinsi mtu anavyojaliwa na Roho
Mtakatifu, Mdo 21:11-14.
ii.
tena unabii unatolewa rohoni mwa mtu, lakini hujulishwa
wengine kwa maneno anayoyachagua mwenyewe, Mdo 20:29-31.
- Unabii wa Roho
Mtakatifu unaleta maneno ya kujenga, kufariji, kutia moyo na hata ukiwa wa
kuonya na kuongoza roho yake ni ya upendo wa Yesu, 1Kor 14:3.
VII.
KARAMA YA KUPAMBANUA ROHO
- Karama hii ni uwezo
maalumu wa Roho Mtakatifu kupambanua roho ndani ya matokeo na maneno mbalimbali
katika watu, Ufu 2:2.
- Katika kupambanua
hivi kuna matokeo ya roho tatu, Mdo 16:16-18, 1Yoh 4:1.
i.
Roho wa Mungu
ii.
roho ya mwanadamu
iii.
roho chafu
VIII.
KARAMA YA AINA ZA LUGHA
- Karama hii
hufunuliwa katika uwezo wa kusema kwa lugha ngeni bila kujifunza, lugha hizo
zinaweza kuwa za wanadamu au za malaika, Mdo 2:4, 11; 1Kor 13:1; 14:2.
IX.
KARAMA YA TAFSIRI YA LUGHA
- Karama hii siyo
maarifa ya kujipatia kwa kujifunza bali ni uweza unaotokea mtu akipewa na roho.
- Mwenye karama hii
anaweza kujaliwa kutafsiri, mwingine akinena kwa lugha, 1Kor 14:27.
- Mtu mwenye karama
hii anaweza kujitafsiri mwenyewe, kusudi wenzake wajengwe akijaliwa na Roho,
1Kor 14:13.